Friday, 14 March 2014

HUYU NDIYE MUIMBAJI ALIYENUSURIKA UPASUAJI KWA KALENDA YA MUNGU


Anastazia Mukabwa katika mojawapo ya matamasha mjini Arusha.
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO, unaweza ukawa unaujua wimbo wa kalenda ya Mungu, lakini hujui umetokana na nini. Lakini ni kwamba dakika chache kabla ya kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua watoto mapacha, ndipo hapo Mungu alipoingilia kati na kugeuza kila kitu na hali ikabadilika.

Siku Annastazia Mukabwa alipopatwa na uchungu na kisha kupelekwa hospitali, akiwa na watoto mapacha tumboni, ndio siku ambayo KWA TAARIFA YAKO wimbo ulipatikana. Akiwa amekaguliwa hata dakika za mwisho madakatari wasione namna ya kufanya kutokana na kueleza kuwa watoto wamekaa vibaya.

Katika hali aliyokuwa nayo, madaktari wanasema walijaribu kila namna pasipo mafanikio, kutokana na njia kutofunguka. Na hata baada yya hapo wakaamua kumuingiza chumba cha upasuaji (theater), ili basi zoezi lianze, KWA TAARIFA YAKO baada ya kutia saini ya kukubali, wakampeleka humo ndani kwa ajili ya zoezi kuanza.


Kabla ya mkasi kupitishwa, aliwaomba madaktari wasubiri kwanza aongee na Mungu, ndipo hapo wakamkubalia, KWA TAARIFA YAKO, hapo ndipo muujiza ulipotokea. Kwani licha ya kuongea kwa sauti tu akiwa hata hajafunga macho, huku madaktari wakimsikia, alimkumbusha Mungu namna ambavyo amemtumikia na ni kwa kiasi gani anahitaji bado kutumika.

Maombi hayo mafupi kwa Mungu yalipoisha, ndipo hapo alipopakwa dawa kwa ajili sasa ya kuanza zoezi, lakini KWA TAARIFA YAKO, wakati Anastazia Mukabwa akiwa hajitambui tayari, daktari mmoja alikosa ujasiri kufikia kiasi hata cha kuangusha mkasi kutoka mkononi mwake, kisha akawaambia wenzake kuwa roho yake haiko tayari kwa ajili ya kufanya upasuaji, na kwamba imekataa kabisa.

Kilichotokea baada ya Anna kuzinduka, ilikuwa ni kushudia ameshajifungua tayari, huku akiwa hajaguswa na mkasi tumboni mwake, KWA TAARIFA YAKO hata madaktari wakakiri na kusema kuwa Mungu yupo, na kwamba ana makusudi na maisha yake ili apate kumtumikia zaidi na zaidi.

KWA TAARIFA YAKO alichokishuhudia Anna ndicho kikapelekea kurekodiwa kwa kalenda ya Mungu, ambapo imedhihirika kuwa licha ya madaktari kuwa tayari kwa zoezi lao la kitabibu, na kuhusu uwepo wa wachungaji pamoja na watu mbalimbali waliokuwa eneo hilo wanaomba, kiufupi ni kwamba, KWA TAARIFA YAKO, kalenda ya Mungu si ya mwanadamu.

Kwa namna ilivyo, huenda hata hapo ulipo umeshanenewa mengi wa watesi wako, wameshasema kuwa huwezi kufaulu shule, hutopata faida kwenye biashara yako, hutokenga nyumba, ama hata kukuambia kuwa hautopata mtoto. Labda tu nikuambie, KWA TAARIFA YAKO, Kalenda ya Mungu si ya mwanadamu, watasema sana lakini hawawezi kuzuia NENO la Mungu na ahadi zake kutimia juu yako

No comments:

Post a Comment