Tuesday, 22 April 2014

PICHA ZA AWALI ZA TAMASHA LA PASAKA JIJINI DAR ES SALAAM...ROZI MUHANDO NA MASANJA NA WALIFANYA VIZURI.

  Karibu tukupe picha za awali za tamasha la kimataifa la Pasaka kama ambavyo huwa linaandaliwa na kampuni ya Msama Promotions. Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake vilipata fursa ya kumsifu na kumuabudu Mungu kwa uimbaji, wakiongozwa na waimbaji nyota barani Afrika. Kekeletso Phoofolo akiwa nahodha.
 Kama kawaida ilikuwepo kwa ajili yako, kama ulitamani kuja lakini hukufanikiwa, pengine ulikuwa 'Canada' au 'Benin', basi picha hizi ni za awali, endelea kutembelea kwa ajili ya picha kedekede za ziada na hata video za tukio hilo. Kama ulikuwepo, basi na tujikumbushe na kisha utuandikie maoni ni muimbaji gani alikugusa sana kwenye tamasha hilo.
Ni mwendo wa mfululizo, wimbo hadi wimbo. Prophet Keke punde baada ya kupanda jukwaani

Monday, 21 April 2014

ASKOFU MACHA WA JCMI ARUSHA ATUMIA IBADA YA PASAKA KUWAASA WAKRISTO JUU YA AMANI YA TANZANIA PAMOJA NA BUNGE LA KATIBA.






                              Askofu Paulo  Macha

Askofu wa makanisa ya JCMI Arusha Bishop Paulo Macha ametumia siku kuu ya pasaka kuwaasa waumini wa makanisa ayo kuombea amani ya Tanzania pamoja na bunge la katiba linaloendelea mkoani Dodoma.

Tuesday, 15 April 2014

MKE WA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEFARIKI NCHINI KENYA AJIFUNGUA MDA MCHACHE BAADA YA MAZISHI YA MUMEWE

Marehemu Peter Kaberere na mkewe enzi za uhai wake.

Mke wa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya marehemu Peter Kaberere ambaye amefariki wiki iliyopita wakati akiosha gari yake, mkewe amejifungua mtoto wa kike masaa machache baada ya mazishi ya mwimbaji huyo siku ya ijumaa iliyopita.

SOMO LA LEO : KIPIMO KIKUBWA CHA MTU MKAMILIFU ..

NENO LA MSINGI:

YAKOBO 3:2:

“Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. MTU ASIYEJIKWAA KATIKA KUNENA, HUYO NI MTU MKAMILIFU, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.”

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><

Viko vipimo kadhaa katika Biblia ambavyo tunaweza kujipima ukamilifu wetu, huku tukijilinganisha na mfano wa mtu mkamilifu, Yesu Kristo [ZABURI 37:37]. Kipimo kikubwa kimojawapo cha ukamilifu ni mtu kuweza kuuzuia na kuutawala ulimi; na kuufanya useme yale tu ambayo Yesu mwenyewe angeweza kuyasema. Biblia inasema kwamba, ulimi wa mtu asiye mkamilifu ni ULIMI MOTO NA ULIMWENGU WA UOVU; nao ndio uutiao mwili wote unajisi, na kuuwasha moto mfulizo wa maumbile [YAKOBO 3:6]. Ikiwa watu wengi katika Kanisa la Nyumbani au Kanisa Kuu, ndimi zao ni moto na ulimwengu wa uovu; basi mwili wote yaani Kanisa lote litatiwa unajisi na kuwashwa moto kwa sababu yao. Moto wa ulimi unaweza kuligawanya Kanisa, na kuleta makundi makundi kuondoa upendo kati yetu na kumfanya Roho Mtakatifu awe mbali nasi. Biblia inasema “Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo[YAKOBO 3:10]. Biblia inazidi kutueleza kwamba, mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, dini yake mtu huyo haifai na anajidanganya moyo wake kwamba ni mkristo [YAKOBO 1:26]. Ikiwa tunataka kufahamika kwamba ni wakristo, basi inatubidi tuwe na ndimi zilizo baridi, zinazotoa baraka wakati wote katika Kanisa, na mataifa wanaotuzunguka.

Friday, 11 April 2014

MTOTO ALIYEPIGWA RISASI YA KICHWA KANISANI, APEWA RUHUSA YA KUTOKA HOSPITALINI BAADA YA MATIBABU

Mtoto Satrine akiwa na baba yake hapo jana, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini ©mobile.nation
Hatimaye mtoto wa mwaka mmoja na nusu Satrine Osinya ambaye risasi ilituhama kichwani kwake baada ya tukio la mtu asiyefahamika kuvamia kanisa mjini Mombasa na kufyatua risasi na kuua watu wawili eneo la tukio na wengine wanne baadae akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo, hapo jana ameruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa chini ya uangalizi wa daktari baada ya kutolewa risasi hiyo.