Askofu Paulo Macha
Askofu wa makanisa ya JCMI Arusha Bishop Paulo Macha
ametumia siku kuu ya pasaka kuwaasa waumini wa makanisa ayo kuombea amani ya
Tanzania pamoja na bunge la katiba linaloendelea mkoani Dodoma.
Bishop Paulo macha ameyasema ayo wakati akifundisha neno la mungu kanisani hapo na kusisitiza waumini
kuwa na moyo wakuliombea Taifa kwani Amani ya nchi imebadirika ikiwa tofauti na
zamani kwani matukio mengi yasiyotegemewa yanajitokeza na kuashiria kupotea kwa
amani nchini.
Waumini wa JCMI wakimsikiliza Askofu kwa umakini
“Ivi sasa baadhi ya makanisa mengi mkoani Dar es salaam
yamebidi kuwekewa ulizi wa polisi kutokana na kuhofia mlipuko wa mabomu
unaojitokeza mara kwa mara na kuashiria kua amani imepotea Tanzania”Alisema
Macha.
Aidha ameongeza kua Mkoa wa Arusha ndio unaongoza kwa
matukio mengi ya ulipukaji wa mabomu na kusababisha vifo vya watu hivyo waumini
wanapaswa kutumia mda mwingi kufunga na kuombea mkoa wa Arusha pamoja na Taifa
kwa ujumla ili amani isipotee.
Pastor Steven Wambura kutoka Dar es salaam
akizungumzia amani ya Tanzania.
“Bungeni nako kumekua na mvutano mkubwa katika uundajii wa katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania na kusababisha mgawanyiko mkubwa kati ya wabunge vyama vya
upinzani na chama tawala na kusababisha ugumu wa kupata katiba ya Nchi hivyo
waumini tunapaswa kusimama kwa makini kuliomba bunge letu”Alisema macha.
No comments:
Post a Comment